Mahakama ya Katiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeidhinisha jana Jumanne sheria inayoruhusu kufanyika kwa kura ya maoni.
Wakosoaji wa serikali wanahofia kuwa hatua hiyo inaweza kutumika kumuwezesha Rais Felix Tshisekedi kugombea muhula wa tatu wa urais.
Akitangaza uamuzi huo jana jioni kupitia televisheni ya taifa Rais wa Mahakama hiyo Dieudonne Kamuleta Badibanga alisema sheria iliyopendekezwa ilikuwa inaendana na katiba.
Vyama vya upinzani vilivyoodhoofika baada ya Tshisekedi kuchaguliwa tena mwaka 2023, vimeungana kupinga jaribio lolote la mabadiliko ya katiba.
Tshisekedi lakini amekana kutaka kuwania awamu ya tatu, ingawa katika mkutano ambao hufanya kwa nadra na waandishi wa habari mwezi Mei alisema itakubaliana na maombi ya watu ikiwa watamtaka agombee kwa awamu ya tatu.