Zaidi ya nusu ya nchi inakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, kulingana na UM

Nchini Sudan Kusini, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) halina uwezo. Kulingana na makadirio ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa, zaidi ya 56% ya wakazi milioni 13 wa nchi hiyo kwa sasa wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.

Njaa inatishia baadhi ya maeneo ya Sudan Kusini kutokana na mapigano mapya na kuvunjika kwa makubaliano ya amani ya mwaka 2018. Wakati shughuli za kibinadamu zikiongezeka kutokana na kufunguliwa tena kwa ufikiaji wa kibinadamu katika baadhi ya maeneo yanayoshikiliwa na upinzani katika wiki za hivi karibuni, WFP inahitaji dola milioni 266 ili kuzuia hali mbaya zaidi.

"Hatari halisi ya njaa"

Kulingana na msemaji wa WFP nchini Sudan Kusini, Tomson Phiri, aliyehojiwa na mwandishi wetu nchini humo, Florence Miettaux, "Programu ya Chakula Duniani inatia wasiwasi mkubwa kuhusu watu wengi waliokwama katika maeneo yasiyofikika ya Sudan Kusini, ambapo njaa na utapiamlo vinaweza kuongezeka." 

"Katika kaunti nne," alisema, "kuna hatari halisi ya njaa ikiwa hali itaendelea kuwa mbaya. Kaunti hizi hazishuhudia chochote ila migogoro hivi karibuni, na wakazi wake wengi wamekwama kati ya mafuriko na mstari wa mbele. WFP iinajaribu kutafuta uwezo ilikukabiliana na hali hii mbaya. Tunafanya kazi kwa bidii ili kupata suluhu. Tunatumia mito, barabara, na usafiri wa anga kujaribu kuwafikia watu wanaohitaji msaada wa chakula."

"Pengo"

Kwa ujumla, Tomson Phiri anasema, "kuna takriban Wasudan Kusini milioni 7.8 wanaohitaji msaada, lakini kutokana na ukosefu wa uwezo zwa kutosha, tunalenga watu milioni 4.2 pekee. Kwa hivyo tayari kuna pengo. Na hata miongoni mwa wale wanaolengwa, bila ufadhili wa ziada, kuna hatari ya kuchukuwa maamuzi magumu."

Na WFP nchini Sudan Kusini inasema inabeba mzigo mkubwa wa vita vya Marekani na Iran, huku kukiwa na kizuizi cha Mlango Bahari wa Hormuz na gharama za mafuta zinazoongezeka, na kusababisha gharama ya ziada ya dola milioni 3.2 kila mwezi kwa shirika hili la Umoja wa Mataifa ambalo tayari linakabiliwa na uhaba wa ufadhili."

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii