Mvutano mpya umeibuka kuelekea Kombe la Dunia 2026 baada ya Iran kulalamikia Marekani kufuta mgao wa tiketi kwa mashabiki wake.
Shirikisho la Soka la Iran limeilaumu Marekani kwa kufuta mgao wake wa tiketi za mechi za hatua ya makundi za Kombe la Dunia, likisema hatua hiyo inawazuia mashabiki wa Iran kuhudhuria michezo ya timu yao nchini humo.
Iran inadai kuwa licha ya kuwa na haki ya kupata asilimia nane ya tiketi kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, mgao huo umeondolewa ghafla mvutano huo unakuja wakati Iran na Marekani zikiwa na uhusiano mbaya wa kisiasa.
Wakati huo huo refa wa Somalia Omar Artan aliyepaswa kuwa wa kwanza wa nchi hiyo kuchezesha Kombe la Dunia amezuiwa kuingia Marekani licha ya kuwa na hati sahihi za kusafiria.
FIFA imesema masuala ya visa yako chini ya mamlaka ya nchi mwenyeji. Haya yanajiri siku chache baada ya Iran pia kuripoti kuwa baadhi ya wafanyakazi wa timu yake wamekatazwa visa za kuingia Marekani, huku timu hiyo ikitarajiwa kuweka kambi yake nchini Mexico wakati wa mashindano.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime