Israel yamuua kamanda mpya wa tawi la kijeshi la Hamas

Israel imetangaza leo kuwa imemuua kiongozi mpya wa tawi la kijeshi la Hamas huko Gaza Mohammed Odeh mauaji hayo yamefanyika baada ya Israel kumuua mtangulizi wa kamanda huyo mapema mwezi huu.

Israel imetangaza leo kumuua kiongozi mpya wa tawi la kijeshi la Hamas huko Gaza Mohammed Odeh baada ya kumuua mtangulizi wake mapema mwezi huu licha ya kuwepo kwa makubaliano ya usitishaji mapigano.

Katika taarifa ya pamoja jeshi la Israel pamoja na shirika la usalama wa ndani la Shin Bet wamethibitisha kuuawa kwa Odeh siku ya Jumanne.

Taarifa hiyo ya pamoja ilisema kuwa, kamanda huyo aliteuliwa kuwa mkuu wa Brigedi za Ezzedine Al-Qassam baada ya kuuawa kwa aliyekuwa kiongozi wake Ezzedine al-Haddad Mei 15,2026.

Hata hivyo kundi la Hamas halikuthibitisha kumteua Odeh kama mkuu wa Brigedi hizo haya yanajiri wakati hali ya tahadhari ikiendelea kushuhudiwa licha ya kuwepo na makubaliano ya kusitisha mapigano katika eneo hilo.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii