Urusi na Ukraine zashambuliana vikali kwa droni, makombora

Urusi na Ukraine zimeendelea kushambuliana vikali usiku kucha kwa kutumia droni na makombora. Mapigano hayo yanaonesha kuendelea kwa mvutano mkali kati ya pande hizo licha ya juhudi za kimataifa za kupunguza vita.

 Kwa mujibu wa taarifa nchini humo mji wa bandari wa kusini mwa Urusi wa Taganrog uliopo katika Bahari ya Azov watu wawili wamejeruhiwa ambapo  Meya wa mji huo Svetlana Kambulova amesema kupitia mtandao wa Telegram kuwa majeruhi hao wamepelekwa hospitalini.

Kwa mujibu wa tovuti huru ya mtandaoni ya Astra, kiwanda cha ukarabati wa ndege kililengwa katika shambulio hilo pia mashambulizi yameripotiwa katika maeneo ya Tuapse, Voronezh na Crimea.

Katika eneo la Crimea ambalo lilinyakuliwa na Urusi mwaka 2014, milipuko imeripotiwa katika mji mkuu Simferopol pamoja na bandari ya kijeshi ya Sevastopol.

Mapigano hayo yanaonesha kuendelea kwa mvutano mkali kati ya pande hizo mbili licha ya juhudi za kimataifa za kupunguza vita vya Ukraine .

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii