Israel imetangaza kwamba imemuua Mohammed Odeh mkuu mpya wa tawi la kijeshi la Hamas katika ukanda wa Gaza katika shambulio lililofanyika Jumanne.
Odeh alikuwa ameteuliwa
hivi karibuni kuchukua nafasi ya Ezzedine al-Haddad aliyeuawa na Israel mapema
mwezi huu licha ya kuwepo kwa usitishaji wa mapigano unaoendelea.
Kwa mujibu wa jeshi la Israel na shirika la usalama wa ndani la Shin Bet Odeh alikuwa akiongoza tawi la kijeshi la Al-Qassam ambalo linahusika na oparesheni za kijeshi za Hamas.
Kifo
chake kinamfanya kuwa kiongozi wa nne wa ngazi ya juu wa Al-Qassam kuuawa tangu
kuanza kwa vita vya Gaza.
Afisa mmoja wa Hamas ameliambia shirika la Habari la AFP kwamba
watoto watatu wa Odeh pia waliuawa wakiwemo wavulana wawili na msichana mmoja
mwenye chini ya umri miaka 18.
Mazishi ya Odeh na familia yake yalifanyika Jumatano katika Gaza
City na kuhudhuriwa na mamia ya waombolezaji.
Hata hivyo tangu shambulio la Hamas dhidi
ya Israel mnamo Oktoba mwaka 2023 Israel imekuwa ikiwalenga viongozi wa kundi
hilo ndani ya Gaza na katika maeneo mengine ya ukanda huo.
Aidha mashambulizi hayo yamekuwa sehemu ya kampeni pana ya kijeshi ambayo Israel inadai inalenga kudhoofisha uwezo wa Hamas wa kufanya mashambulizi.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime