Mkuu wa jeshi azuia shughuli za Nation Media Group

Shirika kubwa zaidi huru la habari nchini Uganda Nation media group limearifu kuwa limewekwa chini ya ulinzi mkali wa kijeshi mapema Jumapili.

Hatua hiyo inafuatia amri iliyotolewa na Mkuu wa jeshi, Jenerali Muhoozi Kainerugaba aliyeamuru kufungwa kwa televisheni, redio na magazeti ya chombo hicho.

Shughuli zimesitishwa hadi itakapotangazwa tena

Kainerugaba, ambaye pia ni mtoto wa Rais Yoweri Museveni, alitangaza kupitia mtandao wa X kwamba vituo vya NTV Uganda na gazeti la Daily Monitor vitafungwa hadi pale atakapotangaza tena kuvifungulia.

Mkuu huyo wa jeshi la Uganda ameeleza wazi kuwa haamini katika uhuru wa vyombo vya habari na kwamba vyombo hivyo vinapaswa kufuata maagizo ya serikali.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii