Timu za uokoaji nchini Venezuela zinaendelea na juhudi za kusaka manusura zaidi kufuatia matetemeko mawili makubwa ya ardhi yaliyolikumba taifa hilo wiki hii.
Idadi ya vifo imeongezeka na kufikia watu 1,450 kufikia Jumamosi na kufanya tukio hilo kuwa miongoni mwa majanga mabaya zaidi kuwahi kuikumba Venezuela katika miaka ya hivi karibuni.
Vikosi vya uokoaji kutoka mataifa mbalimbali vimewasili katika jimbo la La Guaira, eneo lililoathirika zaidi katika nchi ambayo tayari ilikuwa inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kisiasa na kiuchumi.
Majengo kadhaa yameporomoka kabisa na kubaki kama rundo la kifusi katika jimbo hilo la pwani, lililoko takriban kilomita 40 kaskazini mwa Caracas.
Rais wa mpito, Delcy RodrÃguez, amethibitisha idadi hiyo ya vifo na kutoa takwimu zaidi kuhusu athari za tetemeko hilo. Amesema watu 3,150 wamejeruhiwa, huku wengine 12,721 wakilazimika kuyahama makazi yao kutokana na uharibifu mkubwa wa miundombinu. Aidha, majengo 774 yameripotiwa kuporomoka, na mamia ya mengine yakiwa katika hali hatarishi.
Serikali ya Venezuela, inayoongozwa na RodrÃguez tangu mtangulizi wake aondolewe madarakani na Marekani katika operesheni ya Januari, iliwashukuru raia waliojitolea kupeleka misaada kwenda La Guaira.
Hata hivyo, baadaye ilizuia matumizi ya barabara inayoelekea jimbonu humo, ikieleza kuwa msongamano wa magari ulikuwa unakwamisha safari za magari ya dharura.