Watoa huduma za uokoaji nchini Venezuela wanaendelea na juhudi za kuwatafuta manusura kutokana na matetemeko mawili makubwa ya ardhi yaliyoikumba nchi hiyo Jumatano.
Vifo vilivyosababishwa na matetemeko hayo hadi sasa ni zaidi ya 1400. Maelfu ya watu wamejeruhiwa na wengine zaidi ya 50,000 hawajulikani waliko.
Msaada wa haraka unahitajika
Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa limesema limechunguza idadi ya watu na taarifa za uharibifu ambapo limebaini kuwa takriban watu milioni 1.6 nchini Venezuela wanaweza kuwa wameathiriwa na janga hilo na wanahitaji makazi ya dharura, maji safi, huduma za afya na mahitaji mengine muhimu.
Kufikia sasa, zaidi ya mataifa 20 yameanza kutoa misaada ya kiutu wakati Umoja wa Ulaya umetenga msaada wa Euro milioni 5 kusaidia operesheni za uokoaji na jamii zilizoathiriwa.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime