DR Congo yafanikiwa kusonga mbele Kombe la Dunia

Timu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa mara ya kwanza imefuzu kuingia katika hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia baada ya kuifunga Uzbekistan mabao 3 kwa 1.

Ushindi huo wa Kongo umeiwezesha kushika nafasi ya tatu katika kundi lake na sasa itamenyana na England katika hatua inayofuata.

Katika kundi jingine, Austria na Algeria zimetinga hatua hiyo kufuatia sare ya ya magoli 3 kwa 3, matokeo yaliyomaliza safari ya Iran.

Argentina yazidi kung'ara

Nayo Argentina imeendelea kung'ara ambapo Lionel Messi alifunga bao lake la sita katika michuano hii, huku England ikifuzu kama kinara wa kundi baada ya kuifunga Panama mabao 2 kwa 0.

Timu za Afrika zimeendelea kufurahia mafanikio, huku karibu zote zikifanikiwa kufika hatua ya pili ya mashindano hayo.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii