Kiongozi wa chama cha mrengo wa kulia nchini Ufaransa, National Rally RN Marine Le Pen amesema atawanai urais wa nchi hiyo katika uchaguzi ujao mwakani.
Kiongozi wa chama cha mrengo wa kulia nchini Ufaransa, National Rally RN Marine Le Pen, amesema katika mahojiano ya televisheni kwamba anakusudia kugombea urais kwa tiketi ya chama chake mwaka ujao.
Kauli yake inafuatia hukumu ya mahakama ya rufaa kuthibitisha ana hatia katika kesi ya ufisadi dhidi yake lakini ikamuondolea marufuku ya kushikilia wadhifa wa umma na kumfanya aweze kugombea akiwa amevaa kifaa cha ufuatiliaji wa kielektroniki kwenye kifundo cha mguu.
Katika mahojiano na televisheni ya TF1 Le Pen pia alirudia mpango wake wa kukata rufaa tena kwa mahakama ya juu kabisa ya Ufaransa mjini Paris, akisema anajiona hana hatia.
Le Pen alikimbia kituo hicho cha televisheni kwamba anataka kutafuta njia zote za kisheria kutetea kutokuwa na hatia kwake katika kesi inayomkabili.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime