Marekani imeshambulia maeneo mbali mbali ya Iran ikifyetuwa makombora 13 wakati Tehran ikishambulia maslahi ya Marekani kwa makombora Bahrain na Kuwait
Marekani imefanya mashambulio mapya kwa kutumia ndege,droni na meli za kivita ikiyalenga maeneo mbali mbali ya Iran na kurudisha mzingiro katika bandari za nchi hiyo.
Kwa mujibu wa kituo cha televisheni ya taifa cha Iran, mashambulio ya usiku wa kuamkia leo yameuwa wanajeshi saba wa kikosi maalum cha Jamhuri hiyo ya Kiislamu na wengine kadhaa kujeruhiwa katika kambi ya kijeshi ya Bambour kwenye mkoa wa Sistan Baluchistan ulioko Kusini mashariki mwa nchi hiyo.Iran na Marekani zaongeza mashambulizi katika mzozo wa Hormuz
Kwa upande mwingine Iran imejibu kwa kushambulia maslahi ya Marekani katika mataifa washirika wake kwenye kanda ya Ghuba na kuapa kuendelea kuufunga mlango bahari wa Hormuz, mpaka Marekani itakapokomesha uchokozi wake.
Jeshi la ulinzi wa mapinduzi ya Kiislamu la Iran, limetishia hivi leo kuzuia shughuli zote za usafirishaji nishati kutoka mataifa ya Mashariki ya Kati kupinga mzingiro wa Marekani.