Baada ya kuachiliwa kwa wafungwa 15, tofauti zinaendelea kati ya Kinshasa na AFC/M23

Nchini DRC, kukabidhiwa kwa wafungwa kumi na watano kwa AFC/M23 kulipokelewa vyema na Qatar na Marekani kama hatua ya kwanza ya kujenga imani katika mchakato wa Doha. Lakini nyuma ya operesheni hii iliyofanikiwa kimfumo, Pande mbili, serikali ya DRC ,a AFC/M23 bado wanatofautiana.

AFC/M23 inapinga muundo wa kundi lililokabidhiwa na inadai kwamba utaratibu uliowekwa haukufuatwa kikamilifu. Muhimu zaidi, orodha mbalimbali zilizoandaliwa wakati wa mazungumzo hazilingani tena, na pande hizo mbili zinaendelea kulaumiana kwa idadi sawa ya watu wanaotakiwa kuachiliwa.

Hapo awali, kuachiliwa kwa watu 15 hakukusuluhisha suala la orodha hizo. Kulingana na AFC/M23, ni watu tisa pekee kati ya 15 waliokuwa miongoni mwa majina 768 yaliyowasilishwa kwa timu ya upatanishi. Kati ya wengine sita, mmoja aliripotiwa kuwa Mganda bila uhusiano wowote na kundi hilo. Wengine watano, waliokamatwa hasa Katanga, Ituri, na Kinshasa, pia hawakuwa kwenye orodha hii.

Hata hivyo, mwezi Aprili, hali ilikuwa tofauti: watu 311 waliodaiwa na AFC/M23 walikuwa wametambuliwa katika magereza ya serikali. Kinyume chake, watu 166 wa serikali walikuwa wametambuliwa miongoni mwa wafungwa wa AFC/M23.

Kutokubaliana kuhusu utaratibu

Hoja ya pili ya mzozo inahusu utaratibu. AFC/M23 inasisitiza kwamba njia iliyokubaliwa ilikuwa Kinshasa, Entebbe, Kisoro, na kisha Bunagana. Watu hao 15 hatimaye walipelekwa Beni, kabla ya kukabidhiwa kwa ICRC na kisha kusafirishwa kupitia Uganda. Benjamin Mbonimpa, katibu mtendaji wa AFC/M23, aliwapokea walipofika.

Kwa hivyo, AFC/M23 inabainisha kwamba utaratibu uliopangwa haukufuatwa. Kwa upande mwingine, Kinshasa, Qatar, na Marekani zinakiri mafanikio ya zoezi hilo na kufuata kwake mchakato wa Doha.

Suala la usawa bado linasalia. AFC/M23 inadai kuwa tayari imewapa wanajeshi na wapiganaji elfu kadhaa kutoka kambi ya serikali. Hata hivyo, majadiliano ya Montreux yalilenga takriban wanajeshi 2,000 hadi 3,000 waliotambuliwa. Hakuna uhamisho zaidi ambao umetangazwa bado. AFC/M23 sasa inadai orodha iliyosasishwa na ratiba sahihi. Na ICRC inarudia kwamba operesheni mpya itahitaji kwanza makubaliano mapya kati ya pande hizo mbili.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii