Staa maarufu wa muziki wa Pop, Justin Bieber, na mke wake Hailey Bieber, Septemba 13, 2026, wameadhimisha miaka minane tangu walipofunga ndoa.
Justin ameadhimisha siku hiyo kwa kushirikisha picha kadhaa akiwa na Hailey, huku wawili hao wakionekana kufurahia muda wao pamoja, ikiwemo kucheza mchezo wa pool.
Akisindikiza picha hizo, Justin ameandika ujumbe wa kimapenzi kwa Hailey akisema, “8 years until infinity… new beginnings. i love you baby. happy anniversary.”
Ujumbe huo, hususan kauli yake ya “New Beginnings” inayomaanisha “mwanzo mpya,” umeibua mjadala miongoni mwa mashabiki, ambao wameanza kujiuliza ikiwa Justin anazungumzia hatua mpya katika maisha yao ya familia au anadokeza kuhusu kurejea rasmi kwenye muziki baada ya kukaa kimya kwa muda.
Justin na Hailey walifunga ndoa ya kiraia mjini New York mwaka 2018, kabla ya kufanya sherehe kubwa ya harusi huko South Carolina mwaka 2019.
Kwa sasa, wanalea mtoto wao wa kiume, Jack Blues Bieber, aliyezaliwa mwaka 2024.
Hivyo, maadhimisho ya mwaka huu yamekuwa ya kipekee kwa mashabiki, hasa kutokana na ujumbe wa Justin kuhusu “mwanzo mpya,” ambao hadi sasa hajaueleza kwa kina kuhusu maana yake.