Wazazi Jijini Mwanza wamesisitizwa kutokomeza Ndoa za utotoni kwa vitendo ikiwemo kuwasikiliza watoto wao na kuwapa mahitaji ya Msingi jambo litakalosaidia kujiepusha na vishawishi.
Afisa Mkuu wa Tume ya Haki za binadamu na utawala bora (THBUB)Chrisantus sylivester Ndibaiukao, akizungumza baada ya kuwapa Elimu wanafunzi wasiopungua 900 wa shule ya mshingi Butimba A na shule ya Msingi Butimba B wilayani Nyamagana, katika Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike yaliyoambatana na ufunguzi wa Club ya Haki shuleni hapo.
Ndibaiukao amesisitiza ushirikiano kati ya Wazazi, walimu na Wanafunzi utasaidia wanafunzi kupata haki zao za Msingi jambo litakalosaidia Kupunguza vishawishi katika jamii
Kwa upande wake Mwalimu wa Malezi wa Shule ya Msingi Butimba 'A' Roseline mganga manegese, amesema Elimu inapaswa kutolewa kwa Wazazi katika kuwalinda watoto wao ikiwemo kuwaepusha watoto wasitazame picha chafu katika mitandao
Baadhi ya wanafunzi Nezia Samwel na Samwel Joseph wamesema wataitumia Elimu waliyoipata katika kukabiliana na vishawishi vinavyopelekea Mimba za utotoni.
Imeandikwa| Martin Mbilinyi