Kauli ya Rais Tshisekedi kwa Wakongomani waishio Urusi yakosolewa

Viongozi mbalimbali wa kisiasa na wa mashirika ya kiraia nchini DRC wameikosoa kauli ya rais Felix Tshisekedi kuhusu kukanusha kifo cha muandamanaji na kutangaza kuipinga Katiba aliokula kiapo kuilinda, pamoja na kuzungumzia kesi ilipo mahakamani, hatua ambayo wanaona inadhihirisha ni kiasi gani vyombo vya sheria havipo huru.

Akizungumza mbele ya raia wa DRC waishio huko Urusi, Rais Felix Tshisekedi alisema kuwa tangu alipoingia madarakani mwaka 2019 hakuna muandamanaji hata mmoja aliyepoteza maisha, akienda mbali zaidi kuzungumzia rikodi ya mtangulizi wake Joseph Kabila kwamba wakati wa utawala wake waandamanji walifuatwa hadi kanisani na kuuawa.

Martin Fayulu kiongozi wa muungano wa Lamuka ameghadhabishwa na kauli hii na kusema kwamba hivi karibuni Manassé Lomboto aliuawa Septemba 15 wakati wa maandamano ya upinzani huko Kinshasa.

Rais wa Lamuka, ambaye msemaji wake ni Pince Epenge, alisisitiza kwamba mwanaharakati huyo alikufa kutokana na shambulio lililoendeshwa na wanamgambo wa chama tawala.

Alidai uchunguzi huru, akisisitiza kuwa hakuna vitisho vitakavyonyamazisha ukweli. Upande wake Jean-Marc Kabund alishiriki hasira hiyo hiyo. Kiongozi wa upinzani anamtuhumu Félix Tshisekedi kwa kuhatarisha kuwashawishi mahakimu wanaochunguza kesi ya Epenge.

Kwa Jean-Claude Katende wa shirika la ASADHO, uingiliaji kati huu wa rais unaonyesha kikamilifu ukosefu wa uhuru wa mahakama ya Kongo.

Mwanaharakati huyo pia anasema amechukizwa sana na kauli ya rais kuhusu kutaka kubadili Katiba, Katiba ambayo aliapa mara mbili kuilinda.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii