Vital Kamerhe apingwa na maafisa wa chama baada ya matamshi yake kuhusu vita Mashariki

Chama cha Vital Kamerhe kinakabiliwa na malumbano ya ndani. Maafisa kadhaa wakuu wa chama cha UNC wamesaini taarifa ya kukanusha matamshi yaliyotolewa na kiongozi wao mwishoni mwa wiki iliyopita. Alilihoji kuhusu umuhimu wa kuendelea na vita mashariki mwa nchi.

Mnamo tarehe 25 Novemba 2026, viongozi kumi na mmoja wa chama UNC nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) walimpinga hadharani kiongozi wao, Vital Kamerhe, baada ya matamshi yake kuhusu vita mashariki mwa nchi hiyo na matumizi ya fedha za jeshi.

Viongozi wakuu wa chama cha Union pour la Nation Congolaise (UNC), wanaojiita "mrengo wa wahafidhina" (Courant des conservateurs), wametoa tamko la kumtaka rais wa chama chao, Vital Kamerhe, kufuta kauli zake alizozitoa hivi karibuni kuhusu vita vya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na uhusiano wake na Rais Félix Tshisekedi

Tarehe 20 Novemba 2026 huko Kinshasa, Vital Kamerhe alihoji kuendelea kwa vita mashariki mwa DRC, akauliza kuhusu uwazi na matumizi ya mabilioni ya fedha za kijeshi, na kusema uaminifu si wa milele

 Akiwa katika mkutano wa chama huko Kinshasa, tarehe 20 Novemba 2026 huko Kinshasa, Vital Kamerhe alihoji uhalali wa kuendelea kwa vita mashariki mwa nchi na matumizi ya mabilioni ya fedha za kijeshi bila mafanikio yanayoonekana. Pia alimtaka Rais Tshisekedi kuwawajibisha viongozi wa jeshi na mawaziri wa ulinzi, huku akionya kuwa utii wake kwa rais si wa milele.

Kundi la makada 11 wakuu wa UNC—wakiwemo wabunge kama Jean-Baudouin Mayo Mambeke, Michel Moto Muhima, na Gaborian Mboma Kumeza, pamoja na Waziri Molendo Sakombi—walisaini tamko la kujitenga na kauli hizo.


 Waliotia saini wamedai kuwa kauli za Kamerhe hazikutokana na mashauriano ya ndani ya chama, haziwakilishi msimamo rasmi wa UNC, na zinaweza kuvunja moyo jeshi (FARDC) pamoja na kudhoofisha umoja wa kitaifa.

 Uongozi wa UNC umeamua kutochukua hatua za kinidhamu mara moja dhidi ya makada hao na badala yake kupendekeza mazungumzo ya ndani pindi Kamerhe atakaporejea nchini.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii