Familia ya Alute Mughwai yakabidhi CHADEMA kuratibu mazishi

Familia ya marehemu Alute Mughwai Lissu, kaka wa Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, imekabidhi chama hicho jukumu la kuratibu shughuli zote za mazishi ya marehemu huyo.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, Aman Golugwa, ametangaza uamuzi huo leo baada ya kikao kati ya familia na viongozi wa chama kilichofanyika usiku, kufuatia mwili wa marehemu kuwasili katika Kijiji cha Mahambe, Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, ukitokea Arusha.

Alute alifariki dunia usiku wa kuamkia Novemba 1, 2026, katika Hospitali ya Selian jijini Arusha, alipokuwa akipatiwa matibabu.

Awali, familia ilisimamisha maandalizi ya mazishi ikisubiri hukumu ya kesi iliyokuwa ikimkabili Tundu Lissu, iliyosomwa Novemba 6, 2026, katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii