Zimbabwe imeibuka taifa la kwanza katika bara la Afrika kuidhinisha chanjo ya kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Zimbabwe itaanza kutoa chanjo hiyo rasmi baada ya kupata idhini ya matumizi yake kutoka kwa wadhibiti.
Chanjo hiyo ya cabotegravir(CAB-LA) hutolewa kwa kipindi cha wiki nne tofauti, ikifuatwa na chanjo ya kila baada ya wiki nane.
Hatua hiyo ya Zimbabwe inakujia baada ya kuidhinisha pete ya ukeni ya kuzuia virusi vya Ukimwi mapema mwaka huu.
Dawa hiyo pia imeidhinishwa na nchi zingine mbili zikiwemo Marekani na Australia.
Kulingana na Shirika la Afya Duniani(WHO), chanjo hiyo ina uwezo wa kupunguza makali ya VVU kwa asimilia 79 ikilinganishwa na tembe.
WHO sasa linapendekeza matumizi ya chanjo hiyo likisema litasaidia pakubwa katika kupigana na jinamizi hilo.