Liz Truss amejiuzulu kama waziri mkuu wa Uingereza baada ya kukaa madarakani kwa chini ya miezi miwili.
Kuanzia mkutano wake wa kwanza na Malkia, hadi machafuko ya bajeti yake ndogo, wiki zake sita madarakani zimekuwa mchanganyiko wa nyakati za kihistoria na migogoro ya kisiasa aliyojiletea mwenyewe.
Hapa kuna matukio sita ya kukumbukwa kwa muda wake mfupi aliyohudumu.
Ingawa ameingia kwenye historia kama waziri mkuu aliyekaa muda mfupi zaidi nchini Uingereza, Bi Truss alipigwa picha kwenye picha ya mwisho ya hadhara na mfalme aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi nchini humo.