Maambukizia ya kifua kikuu yaongezeka duniani

Ripoti mpya ya Shirika la Afya Ulimwenguni WHO, inasema dadi ya watu walioambukizwa ugonjwa wa kifua kikuu, ikiwa ni pamoja na uwepo wa wenye kupata usugu wa dawa, imeongezeka kwa mara ya kwanza baada ya miaka kadhaa.

Shirika hilo limesema kwa mwaka 2021 zaidi ya watu milioni 10 duniani kote wamefikwa na maradhi ya kifua kikuu, ikiwa ni ongezeko la asilimia 4.5 ikilinganishwa na mwaka uliopita. Ripoti inasema takribani watu milioni 1.6 wamekufa.

WHO inasema kiasi ya visa 450,000 vimehusishwa na usugu wa madawa ya ugonjwa huzo, ikiwa ni ongezeko la asilimia 3, kwa ulinganifu wa mwaka 2020. Janga la Uviko limevuruga huduma kwa watu wenye ugonjwa wa kifua kikuu, ikiwa sawa na progamu nyingine. Shirika hilo limesema watu wengi walishindwa kugunduliwa, jambo ambalo limesababisha idadi ya maambukizi mapya yaligunduliwa kupungua kutoka watu milioni 7 kwa 2019 hadi milioni 2020.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii