Rais Samia Suluhu Hassan amempokea Rais wa Kenya, William Ruto na kumkaribisha Ikulu Dar es Salaam ambapo watazungumzia masuala kadhaa ya ushirikiano ukiwamo ya kibiashara.
Rais Ruto aliwasili nchini jana Jumapili Oktoba 9, 2022 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili akiambatana na mke wake Rachel pamoja na maofisa wa Serikali na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Stegomena Tax.
Leo Oktoba 10 Rais Samia amempokea Rais Ruto na kumkaribisha Ikulu ya Dar es Salaam ambapo baada ya mazungumzo yao ya ndani wanatarajiwa kuzungumza na vyombo vya habari.