Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov amesema jana kwamba hakuwa na taarifa kuhusu mlipuko uliotokea nchini Poland. Alipoulizwa swali na shirika la habari la Reuters kuhusu mlipuko huo, Peskov alisema kwa bahati mbaya hana taarifa zozote.
Wizara ya ulinzi ya Urusi pia imekanusha kuwa makombora ya nchi hiyo yalivuka mpaka wa Ukraine na kuipiga Poland. Ripoti hizo za jana Jumanne zimeibua wasiwasi mkubwa na miito imetolewa kubaini hasa ni kitu gani kilichotokea.