Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi amemteua Dk Sharifa Omar Salim kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Ununuzi na Uondoshaji wa Mali za Umma.
Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Novemba 16, 2022 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Zanzibar, Mhandisi Zena A. Said imesema Dk Sharifa ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).
Pia, Dk Mwinyi amemteua Dk Hashim Hamza Chande kuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anaeshughulikia Mipango, Fedha na Utawala katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).