Mwanafunzi mkongwe zaidi duniani afariki

Mwanafunzi mkongwe zaidi duniani wa shule ya msingi, Priscilla Sitieni, ambaye hamu yake ya kupata elimu akiwa katika umri wa zaidi ya miaka 90 iliwavutia watengeneza filamu wa Kifaransa na kupata sifa kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), amefariki dunia nchini Kenya akiwa na umri wa miaka 99.


Mjukuu wake, Sammy Chepsiror, aliliambia gazeti la 'The Standard' kwamba Gogo Priscilla (Bibi Priscilla), kama alivyojulikana sana, alifariki akiwa nyumbani kwake  Jumatano ya Novemba 16, 2022 baada ya kupata matatizo ya kifua.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii