Canada kuleta wahamiaji milioni 1.5 ifikapo 2025

Canada inaweka dau kubwa juu ya uhamiaji ili kujaza pengo katika uchumi wake lililoachwa na watu wanaozeeka wanaoacha kazi - lakini sio kila mtu yuko tayari kuleta watu wengi kutoka ng'ambo.


Mapema mwezi huu, serikali ya shirikisho ilitangaza mpango mkali wa kuchukua wahamiaji 500,000 kwa mwaka ifikapo 2025, na karibu wahamiaji wapya milioni 1.5 wanakuja nchini katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.


Mpango huu utashuhudia  Kanada ikikaribisha takribani mara nane idadi ya wakazi wa kudumu kila mwaka - kwa kila idadi ya watu - kuliko Uingereza, na mara nne zaidi ya jirani yake wa kusini, Marekani.

Lakini kura ya maoni ya hivi majuzi inaonyesha kuwa pia kuna wasiwasi juu ya kukaribisha wageni wengi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii