Mwanamume Mwenye Wake 12 na Watoto 102 Ashindwa Kuhudumia Familia

Mwanaume mmoja kutoka nchini Uganda ambaye ana wake 12 na watoto 102 anaomba msaada wa kukimu familia yake akitaja hali ngumu ya maisha kutoka na uchumi. Read more: https://kiswahili.tuko.co.ke/familia/484148-baba-wa-watoto-102-na-wake-12-aomba-msaada-kulisha-familia/


Musa Hasahya amabe ni raia wa Uganda amejitokeza hadharani kuomba msaada wa kulea familia yake kutokana na kushindwa kuhumia.  


Musa Hasahya, sasa anaiomba serikali na shirika la hisani la Wasamaria Wema kumsaidia akisema familia yake imekuwa mzigo kutokana na kupungua kwa uzalishaji wa chakula.


 Mfanyabiashara huyo ambaye ni babu wa wajukuu 567, anamiliki shamba la ekari 160 ambalo limekuwa likimwezesha kuzalisha chakula cha familia yake kubwa lakini hali ya sasa kiuchumi imefanya kuwa vigumu kwake kusomesha watoto wake
Hasahya anaishi katika shamba hilo na familia yake kubwa ambao wamesambaratika kama wakimbizi.


Babu huyo ambaye mwanawe wa mwisho ana umri wa miaka sita, pia ana vitukuu na wanawe 35 wa kiume pia wameoa na wana watoto. Kati ya wake zake 12, wawili walimtoroka kwa sababu ya hali ngumu ya maisha na kuwacha nyuma watoto 10.
 Hasahya pia kwa sasa ana watoto 98 waliosalia hai kati ya 102. Hasahya, ambaye aliwacha shule akiwa na umri wa miaka 16, alimuoa mke wake wa kwanza Hanifa Hasahya mwaka wa 1971 na kujaliwa mwanao wa kwanza mwaka wa 1973.


Hanifa Hasahya alimsifu mume wake akisema sio mbishi kama wanaume wengine na hushughulikia mahitaji yao na kutoa mashauri kwa yeyote anayemkiuka. Kama njia ya kutekeleza nidhamu katika familia yake, Hasahya alisema huandaa mkutano kila mwisho wa mwezi ambapo huwahesabu watoto wake wote na kusikiliza shida zao kabla ya kuwashauri.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii