Marais wa kikanda kukutana Angola kusaka amani ya mashariki mwa DRC

Mkutano wa marais wa nchi za kikanda unafanyika leo katika mji mkuu wa Angola, Luanda katika juhudi za kutafuta ufumbuzi wa ghasia za umwagaji damu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Tangazo la ofisi ya rais wa Angola limesema rais huyo Joao Lourenco amewaalika rais wa Kongo Felix Tshisekedi na Paul Kagame wa Rwanda, pamoja na mpatanishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta, na pia mwenyekiti wa sasa wa jumuiya hiyo, rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye.

Tangazo la ikulu ya Burundi limethibitisha leo kushiriki kwa Rais Ndayishimiye katika mazungumzo hayo. Katika mkutano na waandishi wa habari jana jioni, msemaji wa Ikulu ya Kinshasa Patrick Muyaya alisema serikali ya nchi hiyo haitakubali kuzungumza na kundi la waasi la M23, hadi pale itakapokuwa imeondoka kikamilifu katika maeneo yote iliyoyakamata kwa mtutu wa bunduki.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii