Papa Francis Afuta Uongozi wa Shirika la Misaada ya Kikatoliki Duniani

Papa Francis  alifuta uongozi mzima wa shirika la Misaada la Kanisa Katoliki kote duniani kufuatia tuhuma za unyanyasaji na udhalilishaji wa wafanyakazi.
Katika uamuzi wake, kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani alimteua kamishna kulisimamia shirika hilo la misaada. Hatua hiyo ya kugutusha ilihusisha maafisa wakuu watendaji wa Caritas Internationalis (CI) lenye makao yake makuu Vatican huko Roma na mashirika 162 ya Kikatoliki ya kutoa misaada, mashirika ya maendeleo na huduma za kijamii yanayofanya kazi katika zaidi ya nchi 200.
Taarifa ya kutimuliwa kwa wakurugenzi wakuu wa CI, ambayo yenye wafanyakazi zaidi ya milioni moja na watu wa kujitolea kote duniani, ilitangazwa katika amri ya papa iliyotolewa na ofisi ya habari ya Vatican.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii