Shirika la Mazingira la Umoja wa Ulaya (EEA) limesema Takriban watu 238,000 katika Umoja wa Ulaya walikufa mapema katika mwaka 2020 kutokana na athari ya uchafuzi wa hewa licha ya uboreshaji wa hewa.
Data mpya zilizotolewa leo Alhamisi zinaonyesha kwamba uchafuzi wa hewa ni hatari kubwa zaidi ya kiafya barani Ulaya na kwa kiasi kikubwa inaathiri afya ya watu haswa katika maeneo ya mijini.
EAA imesema juhudi zaidi zinahitajika ili kufikia lengo la uchafuzi sifuri kufikia mwaka 2050, la kupunguza uchafuzi wa hewa kwa viwango ambavyo havizingatiwi tena kuwa hatari kwa afya.