Rais wa Brazil Jair Bolsonaro amezungumza kwa mara kwanza jana Jumanne tangu aliposhindwa uchaguzi na kutoa hotuba fupi ambayo hakutamka wazi kuyakubali matokeo.
Hotuba yake haikugusia chochote kuhusu matokeo ya uchaguzi wa Jumapili iliyopita lakini akisema tu kwamba ataendelea kufuata sheria za katiba ya nchi hiyo. Hata hivyo baadae mkuu wake wa utumishi Ciro Nogueira aliwaambia waandishi wa habari kwamba Bolsonaro amemruhusu kuanza mchakato wa kipindi cha mpito. Bolsonaro alishindwa kwenye uchaguzi huo kwa asilimia 49.1 dhidi ya mpinzani wake rais wa zamani Luis Inacio Lula da Silva aliyepata asilimia 50.9.