Tumbili Ahudhuria Mazishi ya Jamaa Aliyemlisha

Peetambaram Rajan mwenye umri wa miaka 56, aliripotiwa kufariki dunia baada ya kupata ugonjwa wa ghafla katika nyumba yake iliyoko huko Batticaloa, Sri Lanka. 


Lakini katika maisha yake yote, alijulikana kwa kulisha tumbili kila siku kwa matunda na biskuti kwani wawili hao walianzisha uhusiano wa karibu sana. Gazeti la News First la Sril Lanka liliripoti katika mazishi yake, rafiki huyo mnyama alipata fursa ya kusema kwaheri yake ya mwisho wakati waombolezaji walipomleta kwenye ibada.



 Mnyama huyo alionekana akiwa amesimama ukingoni mwa jeneza la marehemu huku akimpapasa kidevu kwa utaratibu.Muda mfupi baadaye, tumbiri huyo alimbusu kwenye paji la uso.Hatimaye, waombolezaji walilazimika kumbeba tumbili huyo aliyekuwa na huzuni kwa upole kutoka eneo la tukio baada ya kujaribu kushika mkono wa rafiki yake kana kwamba anajaribu kumuamsha.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii