Wakenya Kuingia Afrika Kusini Bila Kuwa Na Visa

Wakenya waruhusiwa  kuingia nchini Afrika Kusini bila visa kuanzia Januari, 1, 2023 kwa muda usiozidi siku 90 kila mwaka


Hii ni baada ya mazungumzo kati ya Rais William Ruto na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa katika Ikulu ya Nairobi siku ya Jumatano, Novemba 9 katika Ikulu ya Nairobi.


Rais Ruto alieleza kuwa sera ya kurudi pia imekubaliwa wakati sheria za uhamiaji zinakiukwa."Kenya inachukulia Afrika Kusini kuwa mshirika wa kimkakati na tumejitolea kujenga uhusiano thabiti wa kiuchumi kati ya mataifa yetu," alisema Rais


Hatua hiyo pia inakujia baada ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kuanzisha majadiliano hayo mwaka wa 2016, akisema kuwa nchi hizo mbili zinahitaji kuondoa masharti ya visa.


Inakumbukwa kuwa Rais Ramaphosa na Uhuru walianza mazungumzo ya kulegeza vikwazo vya visa mwaka wa 2021, kwa Wakenya wanaozuru Afrika Kusini.
Hata hivyo, hii ilitolewa kwa sharti kwamba Kenya iwarudishe maelfu ya raia wake ambao waliingia Afrika Kusini kinyume cha sheria.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii