Polisi Nchini Kenya wamemkamata kijana mwenye umri wa miaka 21 Jared Opiyo Nyatumba kwa kuvaa mavazi ya kike na kutumia jina la kike la mwanamke mwingine ambae ni Sheila Bichange.
Kijana huyo aliwaambia polisi hao kuwa yeye huvaa nguo za wanawake kwa kuwa, ana maumbile ya kike tangu utotoni.
"Alidai kwamba amekuwa na tabia za kike tangu utotoni ndipo akaamua kuvaa kama mwanamke.
Polisi walikuta anakaa kama mwanamume na kumuamuru kuvua nguo hizo.Mara tu baada ya wenyeji wa Awendo kupata habari kwamba mwanamume aliyejidai kuwa mwanamke amekamatwa na polisi, walifululiza kwenye kituo hicho na kutaka wamuone.
Imeibuka kwamba mshukiwa huyo amehusishwa na visa vya mauaji kadhaa, yanayotekelezwa na mtu anayejifanya kuwa mwanamke na kutaka kumfunza adabu."Wenyeji walipata kumuona mshukiw ahuyo kupitia dirisha la ofisi ya kutoa maelezo, ila wakasisitiza aachiliwe ili wampige kitutu" .