Mtoto Wa Museveni Sasa Asema Hataki Tena Kuwa Rais wa Uganda

Mtoto Rais wa Uganda Yoweri Museveni - Jenerali Muhoozi Kainerugaba - sasa anasema kuwa hana haja yoyote ya kuwa rais wa nchini hiyo. 

Licha ya kushiria mara kadhaa na hata kusema kuwa angependa kuiongoza Uganda, Jenerali Muhoozi sasa amebadili ngoma akisema kuwa tayari yeye ni kiongozi na hahitaji urais tena. 


"Watu wengine wanasema kila mara kuwa ninataka kuwa rais. Kusema ukweli hilo halijawahi kuwa akilini mwangu. Tayari mimi ni kiongozi wa kizazi changu. Hiyo ndio heshima kubwa zaidi ninaweza kuwazia. Na kizazi chetu kitakuwa bora zaidi," Muhoozi alisema.



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii