Makamu wa rais wa bunge la Ulaya avuliwa madaraka

Makamu wa Rais wa Bunge la Ulaya Eva Kaili amevuliwa madaraka yake kufuatia kuhusishwa kwake na uchunguzi wa ufisadi na utakatishaji fedha nchini Ubelgiji.Kaili, ambaye anawakilisha Ugiriki, alikamatwa jioni ya Ijumaa nchini Ubelgiji, pamoja na washukiwa wengine kadhaa, katika uchunguzi wa washukiwa wa rushwa.Msemaji katika Bunge la Ulaya amesema Rais wa bunge hilo, Robberta Metsola ameamua kusimamisha maramoja majukumu yote yenye kumuhusu Kaili, kama Kama Makamo wa Rais wa Bunge la Umoja wa Ulaya.Uamuzi wa kumwondoa Kaili, mwenye umri wa miaka 44, kutoka nafasi ya makamu wa rais inaweza tu kutolewa na bunge lenyewe. Ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma imesema mamlaka itakutana baadae kuamua ikiwa washukiwa hao watano, akiwemo Kaili, watasalia ndanichini ya ulinzi au la.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii