Japo alikuwa mwanafunzi ambaye alikwenda Russia kwa ufadhili wa elimu ya juu, Lemekani alihukumiwa kifungo cha miaka 9 jela kwa makosa ya ulanguzi wa dawa za kulevya mnamo Aprili mwaka 2020.
Alisamehemewa baadaye kupitia mpango maalum wa serikali wa kutoa msamaha kwa masharti kwamba angekubali kushiriki katika vita nchini Ukraine, na aliuwawa akiwa katika mapigano.
Waziri wa mambo ya nje wa Zambia Stanley Kakubo amesema kwamba serikali ya Zambia imeiomba Russia kutoa maelezo zaidi kuhusiana na kifo cha Lemekani