Elon Musk ametangaza kuwa anamshtaki mmiliki wa akaunti ya Twitter inayofuatilia ndege yake ya kibinafsi. Musk alisema vitendo hivyo vilimweka mtoto wake hatarini.
Akauti ya @ElonJet ambayo ina wafuasi zaidi ya nusu milioni, ilisimamishwa Jumatano.
Mmiliki wake, Jack Sweeney mwenye umri wa miaka 20, alitumia taarifa za safari za ndege zinazopatikana hadharani kutuma ujumbe kwenye Twitter kila wakati ndege ya Musk ilipopaa na kutua.
Musk alisema kesi zimefunguliwa dhidi ya Sweeney na watu wengine ambao hawakutajwa.
“Jana usiku, gari lenye lil X (hili ni jina la mtoto wa Musk) huko Los Angeles lilifukuzwa (wakifikiri ni mimi) na kichaa ambaye alifunga barabara ya gari na kupanda juu,” Musk aliandika kwenye Twitter.
Aliongeza kuwa akaunti yoyote ambayo inaonyesha mahali walipo watu kwa wakati halisi itazuiwa kwa sababu, kwa maoni yake, inaleta tishio kwa usalama wao wa kimwili