Mwanamuziki mahiri wa Rhumba, Le General Defao Matumona amefariki dunia akiwa nchini Cameroon. Defao ni mwanamuziki mwenye kipaji cha kutunga na kuimba kwa sauti nyembamba na nyororo alijizolea umaarufu mkubwa kupitia nyimbo zake za miondoko ya kucheza Kama vile Ndombolo na Ekibinda nkoi, alizaliwa Disemba 03, 1958, Kinshasa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.