SOMA KWA FURAHA INITIATIVE YAANZA MWAKA 2026 NA CHUMBA CHA TUMAINI ( CHAMBER OF HOPE )

Wazazi na walezi mkoa wa Mwanza wameaswa kusimamia malezi bora na shirikishi kwa lengo la kuwakinga watoto na shughuli ama mambo mbalimbali yanayoweza kuwa hatarishi 

Hayo yameelezwa na Micky Milliam Mkurugenzi na Muanzilishi wa Taasisi ya Soma Kwa Furaha Initiative wakati akizungumza katika  Chamber Of Hope ( Chumba Cha Tumaini ) 

“ Kwa asilimia kubwa kumekuwa na changamoto kwenye jamii zetu haswa upande wa wazazi na walezi kushindwa kutoa elimu bora ya malezi kwa watoto wao, mfano unakuta mzazi hawezi hata kumueleza mtoto kuhusu afya ya uzazi na mambo mengine kama hayo kwamba nini afanye nini asifanye, iyo inaenda mbali zaidi hadi kwa walimu wakati mwingine watoto wanapitia changamoto hata mashuleni na hawawezi kusema hata kwa walimu wao “

Kwa upande mwingine Clara Nour Ayoub ambae ni Afisa Maono ( Vision Officer ) kutoka Taasisi ya Soma Kwa Furaha Initiative ameeleza juu ya umuhimu wa Chamber Of Hope ( Chumba Cha Tumaini ) 

“ Chamber Of Hope ni sehemu sahihi kwa wadau wote kwa sababu mapato yote yanayopatikana hapa yanakwenda moja kwa moja kuchangia na kusaidia watoto walio kwenye makundi maalumu kwa hivo kila ulichochangia hapa kina msaada na  unapaswa kujivunia“

Chamber Of Hope ( Chumba Cha Tumaini ) ni programu inayoratibiwa na Taasisi ya Soma Kwa Furaha Initiative, ikiwa na lengo kuu la kuwakutanisha volunteers na wadau mbalimbali wanao shiriki kusaidia watoto walio katika makundi maalumu .

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii