Wadephul, Rubio kujadili tisho la Trump kuchukua Greenland

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Johann Wadephul anakutana siku ya Jumatatu na mwenzake wa Marekani Marco Rubio mjini Washington kuhusu vitisho vya Marekani kuchukua Greenland hata kwa nguvu.

Aidha Wadephul na Rubio pia wanatarajia kujadili suala la usitishaji vita nchini Ukraine na juhudi za kuisaidia ili kujilinda dhidi ya uvamizi mkubwa wa Urusi.

Kabla ya kuanza safari yake Wadephul aliikumbusha Marekani kuhusu wajibu wake wa kulinda uhuru kujitawala na kuunga mkono jumuiya ya kujihami ya NATO.

Rais wa Marekani Donald Trump anataja umuhimu wa kimkakati wa Greenland uwepo mkubwa wa meli za Urusi na China katika eneo hilo pamoja na rasilimali asilia za kisiwa hicho kama sababu za vitisho vyake.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii