Raia wa Uganda wapewa likizo ya siku 2 za uchaguzi

Katika jiji kuu la Kampala, baadhi ya wakaazi wameanza kusafiri kwenda vijijini au Charo kwa lugha ambayo wanaielewa kushiriki kura za Alhamisi.

Serikali ya Uganda imetangaza likizo ya siku mbili ili kuwapa wananchi nafasi ya kushiriki uchaguzi mkuu siku ya alhamisi wiki hii, katika uchaguzi ambao rais Yoweri Museveni atashindana na kinara wa upinzani, Robert Kyagulanyi.

Katika jiji kuu la Kampala, baadhi ya wakaazi wameanza kusafiri kwenda vijijini au Charo kwa lugha ambayo wanaielewa kushiriki kura za Alhamisi.

Tayari waangalizi kutoka Umoja wa Afrika Jumuiya ya Madola, IGAD na hata ukanda wa maziwa makuu wamewasili nchini humo ili kufuatilia uchaguzi huo muhimu.

Deo Mwapinga ambaye ni Katibu Mkuu wa waangalizi wa maziwa makuu amesema Misingi ya demokrasia katika uchaguzi inaelezwa na sheria za ndani za nchi, iwe ni katiba ya nchi, sheria za uchaguzi akisisitiza kuwa matarajio yao ni kuona wadau wote wa ndani wataheshimu sheria hizo.

Tume ya uchaguzi nchini Uganda imeorodhesha wapiga kura zaidi ya milioni 21 wanaotarajiwa kushiriki zoezi hilo. 

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii