Tahadhari yatolewa kuhusu mauaji ya halaiki Iran

Shirika la kutetea haki za binadamu la Iran lenye makao yake nchini Norway limesema mamlaka za Iran zimefanya mauaji ya halaiki.

Hayo yamesemwa na kundi la haki za binadamu siku ya Jumapili huku serikali ikiamuru maandamano ya kujibu ili kurejesha utulivu.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Iran lisilo la kiserikali Iran Human Rights (IHR) lenye makao yake makuu nchini Norway lilisema limethibitisha mauaji ya waandamanaji wasiopungua 192 lakini likaonya kwamba idadi halisi ya vifo inaweza kufikia mamia kadhaa au hata zaidi. 

Kwa mujibu wa kundi la haki za binadamu lenye makao yake makuu Marekani kwa takriban waandamanaji 490 na wanajeshi 48 wameuawa.

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kufanya mkutano na maafisa wake wakuu siku ya Jumanne kujadili njia za kujibu maandamano nchini Iran.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii