Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Joseph Daudi Mwakalinga maarufu kama @jiggerman mkazi wa Zimbili Kinyerezi Wilaya ya Ilala, kwa tuhuma za kumjeruhi mtoto wake ambaye jinam lake (limehifadhiwa) kwa kutumia fimbo na moto.
Tukio hilo linadaiwa kutokea Januari 08 mwaka huu katika eneo la Kinyerezi ambapo mtuhumiwa anadaiwa kutenda kitendo hicho kinyume na sheria na haki za mtoto.
Jeshi la Polisi limeeleza kuwa hatua zaidi za kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi ya mtuhumiwa kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za kisheria huku uchunguzi ukiendelea ili hatua stahiki zichukuliwe kwa mujibu wa sheria.
Aidha, Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wazazi, walezi na wananchi kwa ujumla kujiepusha na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto, na kuheshimu haki zao kwa kuzingatia sheria, maadili na misingi ya malezi bora.
