Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amesema siku ya Jumatatu kwamba hali nchini humo imedhibitiwa kikamilifu baada ya ukandamizaji wa kikatili wa maandamano ya nchi nzima.
Abbas Araghchi amesema maandamano yaligeuka kuwa ya vurugu na ya maafa ili kumpa Rais wa Marekani Donald Trump sababu ya kuingilia kati.
Hata hivyo hakutoa ushahidi wowote kuhusu kauli zake ambazo zilijiri baada ya wanaharakati kuripoti kwamba zaidi ya watu 500 wameuawa nchini humo katika maandamano hayo yaliyoanza wiki mbili zilizopita.
Rais Donald Trump amesema Iran inataka mazungumzo na Marekani baada ya kitisho chake cha kushambulia Jamhuri hiyo ya Kiislamu kufuatia ukandamizaji wake dhidi ya waandamanaji
Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz amesema ukandamizaji wa Iran dhidi ya waandamanaji ni 'ishara ya unyonge'.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime