Mmiliki wa Twitter Elon Musk anawaomba watumiaji wa mtandao huo wa kijamii kupiga kura kuhusu mustakabali wake kama afisa mkuu mtendaji wake.
Katika kura ya maoni kwa watu milioni 122, kwa watu wanaonifuatilia aliandika kwenye twitter: “Je, nijiuzulu kama mkuu… nitatii matokeo…”
Tajiri huyo wa teknolojia, ambaye pia anamiliki Tesla na Space X, amekosolewa vikali tangu achukue Twitter.
Baada ya mzozo mkubwa wa kisheria, Bw Musk alichukua udhibiti wa kampuni hiyo mwezi Oktoba kwa mkataba wa $44bn (£36bn).
Hatua hiyo inakuja huku Twitter ikisema itafunga akaunti ambazo zimeundwa ili tu kukuza majukwaa mengine ya mitandao ya kijamii. Hatua hiyo pia itaathiri akaunti zinazounganisha au zilizo na majina ya watumiaji kutoka kwa majukwaa kama vile Facebook, Instagram, Mastodon, Truth Social, Tribel, Nostr na Post, kampuni hiyo ilisema kwenye Twitter.
Lakini uchapishaji wa maudhui yanayoweza kusomwa kutoka kwa tovuti zingine bado utaruhusiwa. Bosi wa zamani wa Twitter Jack Dorsey, ambaye hivi karibuni aliwekeza Nostr, alijibu chapisho la Twitter kwa neno moja: “Kwa nini?”.
Katika jibu kwa mtumiaji mwingine anayechapisha kuhusu marufuku ya ukuzaji wa Nostr, Dorsey alisema, “haina maana”.
Siku ya Jumamosi, ripota wa Washington Post Taylor Lorenz alisimamishwa kazi kwa kuvunja sheria hiyo mpya kabla ya kutangazwa rasmi.
Baada ya kuweka link siku ya Jumapili kwenye twitter aliyodai ilizuiliwa.