Wabunge wa Ubelgiji washindwa kuafikiana namna ya kuomba msamaha dhidi y audhalimu wa kikoloni

Wabunge nchini Ubelgiji wameshindwa kuafikiana namna bora ya kupata maridhiano dhidi ya udhalimu wa enzi ya ukoloni baada ya Uholanzi kuomba radhi kwa niaba ya serikali yake kutokana na dhima yake katika biashara ya watumwa iliyodumu kwa miaka 250.

Bunge la Ubelgiji liliunda tume mwaka 2020 katikati ya maandamano makubwa yaliyochochewa na vuguvugu na Black Lives Matter kuchunguza rekodi ya taifa hilo kwenye makoloni yake ya zamani Afrika ya Kati.

Hata hivyo jopo hilo limekiri kushindwa kuafikiana juu ya namna ya kuomba radhi kutokana na matendo yaliyofanywa na uliokuwa utawala wa Ubelgiji huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda na Burundi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii