WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, azungumza na Wakuu wa Vyombo vya Usalama vya Wizara yake katika kikao kazi kilichofanyika Ofisi ndogo ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam, leo Disemba 21, 2022. Kushoto meza kuu ni Katibu Mkuu, Kaspar Mmuya, na kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Maduhu Kazi.