Idadi ya maambukizi ya VVU yaongezeka barani Ulaya

Leo Disemba mosi ni maadhimisho ya siku ya kupambana na UKIMWI Duniani. Shirika la Afya Duniani, WHO pamoja na ofisi ya shirika hilo katika Umoja wa Ulaya yamesema kuwa watu zaidi wanaishi na virusi vya UKIMWI barani Ulaya, bila ya kupimwa wala kugundulika.

Kwa mujibu wa WHO, mwaka 2021, takribani watu 300 waligundulika kuwa na VVU kila siku katika nchi 46 kati ya 53 za Ulaya. Ripoti hiyo inaonesha pia kuwa bado kuna unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI, VVU na kwamba suala hilo linapaswa kukemewa. Mkurugenzi Mkuu wa WHO barani Ulaya, Hans Kluge amesema wanapaswa kuwa na wasiwasi mkubwa kutokana na takwimu za upimaji wa VVU, matibabu na huduma. Kluge anasema kuendelea kuenea kwa unyanyapaa dhidi ya VVU kunawazuia watu kupima na kunawafanya wasifikie lengo lao la mwaka 2030 la kuumaliza kabisa ugonjwa wa UKIMWI.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii