Polisi Dar wamuita Mwingira kwa mahojiano

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro ameagiza ndani ya saa 24 kutafutwa na kuanza kuhojiwa kwa Askofu wa Kanisa la Efatha, Nabii Josephat Mwingira.

Limefikia hatua hiyo baada ya tuhuma mbalimbali zilizotolewa na Mwingira dhidi ya Serikali ikiwamo njama za maofisa wa Serikali kutaka kumuua.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu  Desemba 27, 2021 Muliro amesema tuhuma alizotoa ni nzito hivyo haziwezi kuachwa bila kufanyiwa kazi.

"Tayari Jeshi la polisi limetoa maelekezo ya kutafutwa Mwingira ili  ahojiwe kwa kina dhidi ya tuhuma alizotoa. Atahojiwa kwa mujibu wa sheria kwa kushirikiana na vyombo vingine vya mifumo ya kisheria," amesema Muliro.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii